Judges 5:12-15

12 a‘Amka, amka! Debora!
Amka, amka, uimbe!
Ee Baraka! Inuka,
chukua mateka wako uliowateka,
ee mwana wa Abinoamu.’

13“Ndipo mabaki ya watu
wakashuka dhidi ya wenye nguvu,
watu wa Bwana,
wakashuka dhidi ya mashujaa wenye nguvu.
14 bKutoka Efraimu wakaja watu, ambao chimbuko lao ni Amaleki;
Benyamini akiwa miongoni
mwa watu waliokufuata.
Kutoka Makiri wakashuka viongozi,
na kutoka Zabuloni wale washikao
fimbo ya jemadari.
15 cWakuu wa Isakari walikuwa pamoja na Debora;
naam, Isakari alikuwa pamoja na Baraka,
wakija nyuma yake kwa mbio
wakielekea bondeni.
Katika jamaa za Reubeni,
palikuwa na kujihoji kukubwa moyoni.
Copyright information for SwhNEN